Joho kuandikisha taarifa kuhusu rabsha katika uchaguzi mdogo Malindi

 

Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho anatarajiwa kuandikisha taarifa kuhusiana na vurugu zilizoshuhudiwa katika uchaguzi mdogo wa Malindi mnamo tarehe 7 mwezi machi hapo kesho.

Hii ni baada ya gavana huyo kukaidi amri hiyo hapo jana pale alipotakiwa kuandikisha taarifa kama alivyoagizwa na wizara ya usalama.

Sasa Joho anatazamiwa kuandikisha taarifa hiyo hapo kesho mchana baada ya kudai ana majukumu mengi ya kikatiba anayohitaji kutekeleza kwa wananchi.

Wabunge wote wa upinzani kutoka eneo la Pwani vile vile wametakiwa kufika kwenye kituo cha polisi cha Malindi kuandikisha taarifa.