Ruto ataka mataifa ya Afrika kuondoa vikwazo vya kibiashara na tamaduni
Naibu rais William Ruto ameyataka mataifa ya Afrika kuondoa vikwazo vya kibiashara na tamaduni ambavyo vinaburuza kukua kwa uchumi wa mataifa ya bara la Afrika.
Akiongea katika kongamano la maafisa wakuu wasimamizi wa mashirika barani Afrika, Ruto amesema kuwa mataifa ya bara la Afrika yanahitaji uwazi katika kuendesha bishara baina ya mataifa hayo ,ili kuona kuwa umaskini unatupwa katika kaburi la sahau.
Ameongeza kwa kupigia mfano miradi ya Kenya ya reli ya kisasa na bandari ya Lamu kwa kusema kuwa miradi hiyo itachangia pakubwa kukua kwa uchumi kwa mataifa ya Afrika ya mashariki na kuimarisha kukua kwa uchumi kwa mataifa ya Afrika ya mashariki.