Droo ya UEFA kufanyika leo

Vilabu nane kutoka mataifa tofauti barani Ulaya vitashiriki katika droo ya kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya hatua ya robo fainali hii leo.
Hafla hiyo itafanyika jijini Nyon,Uswizi ambapo itakua wazi kumaanisha timu za nchi moja zinaweza kukutanishwa.
Upo uwezekano wa mibabe kutoka Uhispania Real Madrid na Barcelona kukutana.
Klabu zilizofuzu kuingia robo fainali ni Atlético Madrid,Bayern Munchen, Barcelona,Benfica,Manchester City,Paris Saint-Germain,Real Madrid na Wolfsburg.
Mechi za Robo Fainali zitachezwa Tarehe 5 na 6 Aprili na Marudiano ni Aprili 12 na 13.