Kutojadiliwa kwa swala la Migingo kwagadhabisha Wakenya

Hisia tofauti zimeanza kuibuka kufuatia mazungumzo ya hapo jana kati ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenziwe Yoweri Museveni kwa kutojadili suala tata la kisiwa cha Migingo katika ziwa Victoria.
Baadhi ya wakenya wanasema kuwa mzozo huo huenda ukaleta vita kati ya mataifa hayo mawili iwapo suala hilo halitatatuliwa mapema.
Itakumbukwa mapema mwezi huu shughuli ya usajili wa wapiga kura katika kisiwa hicho zilitatizwa kwa muda kufuatia vuta ni kuvute ya maafisa wa Kenya na Uganda.