Siku ya maji duniani yaadhimishwa leo

 

Wakenya hii leo wanaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya maji ulimwenguni.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni maji na changamoto za kupata ajira katika mataifa mbali mbali ikiwemo Kenya.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa asilimia 50 ya watu wanafanya kazi katika sekta ya maji.

Mwenyekiti wa shirika la kuhufadhi maji na mabomba daktari Julius Kones amesema kuwa wanapania kushirikiana na sekta ya kibinafsi ili kuhakikisha uhaba wa maji unazikwa katika kaburi la sahau.