Tawi jengine la duka la uchumi lafungwa

 

Wafanyikazi na wauzajiwa wa bidhaa katika maduka ya jumla ya uchumi mjini Eldoret wamelalamikia hatua ya kufungwa kwa tawi la duka hilo mapema hii leo mjini Eldoret bila kuwepo kwa ilani.

Baadhi ya waliozungumza na vyombo vya habari wamesema kufungwa kwa baadhi ya maduka hayo kutapelekea vijana wengi kukosa ajira kuitaka serikali kuhakikisha waliochangia kufungwa kwa maduka hayo wafunguliwe mashtaka.