Jopo lasisitiza kuwa Dominic Otieno alipokea matibabu yanayofaa

Jopo lililoundwa na gavana wa Nairobi dakta Evans Kidero kuchunguza kifo tatanishi ya mtoto Dominic Otieno katika hospitali ya Mama Lucy kaunti ya Nairobi, kimesema kuwa mtoto huyo alipata matibabu yanayofaa.
Katika kikao na waandishi wa habari jijini Nairobi, mwenyekiti wa jopo hilo Philip Kungu amesisitiza kuwa hospitali ya Mama Lucy iliwajibika vilivyo katika kumpatia matibabu yanayotakinana marehemu Dominic Otieno.
Kauli ambayo inakizana na ya wazazi wa Dominic, ambao walilaumu hospitali hiyo kwa kutowajibika na kusababisha kifo cha mtoto wao.
Mwenyekiti huyo aidha ametaja ukosefu wa magari ya kusafirisha wagonjwa na ukosefu wa vifaa vya matibabu kama baadhi za changamoto zinazokumba hospitali ya Mama Lucy.