CORD yailaumu Jubilee na IEBC kwa kupuuza juhudi za Okoa Kenya

Muungano wa CORD umelaumu muungano wa Jubilee na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kwa kupuuza juhudi zao za ‘Okoa Kenya.’
Kinara Raila Odinga amesema muungano wake umepeleka sahihi milioni 1.6 mwaka uliopita Novemba na bado hawajapata jibu kutoka kwa IEBC.
Raila amesema walikuwa wanafaa kupata majibu kutoka kwa tume hiyo katika muda wa siku 90 baada ya kuwasilisha sahihi hizo.