Nandwa ateuliwa kuwa kocha mkuu wa Thika United

Klabu ya Thika United imemteua mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa Harambee Stars James Nandwa kama kocha wake mkuu.
Nandwa ambaye hakuwa na shughuli zozote za ukufunzi baada ya kutimuliwa kutoka klabu ya Shabana na kuchukua hatamu za ukufunzi kutoka kwa Moses Irungu ambaye ametimuliwa.
Wanamaziwa hao wamesalia bila usindi tangu kuanza kwa ligi ya taifa na malengo makuu ya Nanwa ni kufufua matumaini ya timu hiyo.
Aidha Nandwa ameweza kuwa mkufunzi waTusker FC , Harambee Stars and AFC Leopards.