FIFA yaishtumu Afrika Kusini kwa kulipa hongo ili kuandaa kombe la dunia 2016

 

Shirikisho la soka duniani FIFA limeishtumu Afrika Kusini kwa kulipa hongo ya dola milioni 10 ili kuruhusiwa kuandaa kombe la dunia la mwaka 2010.

Ripoti ya gazeti moja nchini Uingereza imefichua kuwa Fifa imekerwa na madai hayo kwamba Afrika Kusini ilitumia njia ya mkato kuandaa michuano hiyo.

Hata hivyo Afrika Kusini imesisitiza kuwa hawakulipa hongo hiyo inavyodaiwa.

Hapo jana,Fifa ilisema itakomboa mamilioni ya fedha zilizochukuliwa kinyume cha sheria na wanachama wa shirikisho hilo pamoja na mashirika mengine ya soka.

Maafisa wa zamani wa shirikisho hilo Chuck Blazer na Jack Warner na Jeffery Webb miongoni mwa wengine wamefunguliwa mashtaka na Fifa imewasilisha stakhabadhi kwa mamlaka ya Marekani kutaka warudishe fedha walizoiba.

Kufikia sasa watu 41 na kampuni kadhaa zimeshtakiwa na mamlaka ya Marekani kuhusu masuala ya ufisadi ambayo yameipelekea Fifa kuwa katika mgogoro tangu madai ya ufisadi kugunduliwa mwezi Mei 2015.

Uchunguzi wa Marekani ulifichua ufisadi ndani ya Fifa inakadiria kwamba mamilioni ya madola yaliibwa kupitia hongo,kiinua mgongo na mipango ya ufisadi iliofanywa na washtakiwa.