Nkaissery aunda bodi ya kumiliki silaha

Waziri wa Usalama wa ndani Joseph Nkaissery amemteua meja mstaafu Enock Sasia kuwa mwenyekiti wa bodi ya kutoa leseni za kumiliki silaha humu nchini.
Nkaissery pia amewateua watu wengine nane watakaohudumu kwenye bodi hiyo ambapo watakuwa wanatathimini na kupitisha watu ambao wametuma maombi ya kumiliki silaha.
Pia bodi hiyo itakuwa na Uwezo wa kupokonya na kutoa kibali cha umiliki wa bunduki.
Walioteuliwa ni Lilian Kiambia, Stanely Omucheyi, Bernice Gathegu, Antony Wahome, William Singoei, George Waiguru, James Ngului and Samuel Kimaru kama katibu wa bodi hiyo.
Wanachama wa bodi hiyo watakuwa katika mamlaka kwa muda wa miaka 3 kuanzia machi 16, 2016.
Bodi hiyo itakuwa na wawakilishi wawili kutoka huduma ya polisi kwa taifa( NPS) ambapo mmoja atatoka kwa ofisi ya upelelezi kwa polisi na mwingine kutoka ofisi ya mkuu wa sheria nchini.
Waziri amesema uteuzi ni kwa mjibu wa katiba kulingana na kifungu cha sheria 3(1) ( 2) na (3) cha sheria za silaha.