Kimemia,Ali na Kosgey wateuliwa

 

Rais Uhuru Kenyatta amemteua aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma,Francis Kimemia kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya shirika la ustawi wa viwanda na ICDC.

Rais pia amemteua waziri wa zamani wa viwanda Henry Kosgey kuwa mwenyekiti wa wakfu wa utalii huku aliyekuwa kamishna wa polisi Hussein Ali akiteuliwa mwenyekiti mpya wa bodi shirikishi ya mashirika yasiyokuwa ya serikali.

Haya yanajiri juma moja tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuteuwa mwanasiasa wa zamani Franklin Bett kuongoza shirika moja la serikali.

Hata hivyo wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahoji kuwa teuzi hizo ni za kuhakikisha Uhuru na Ruto wapata uungwaji mkono katika uchaguzi mkuu ujao.