Viongozi waomboleza kifo cha Ayah

images (7)

Rais Uhuru Kenyatta ameomboleza kifo cha aliyekuwa waziri wa maswala ya nje Wilson Ndolo Ayah aliyefariki katika hospitali ya Agha Khan.

Uhuru amemtaja mbunge huyo wa zamani ambaye alifariki katika hospitali ya Aga Khan akiwa na umri wa miaka 84 kama mchapa kazi aliyetumikia nchi yake kama kiongozi shujaa.

Ameongeza kuwa Ayah aliheshimika na alikuwa mnyenyekevu kwa yeyote aliyemfahamu kutokana na ujasiri wake uliochangia pakubwa katika utendakazi wake kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Naye kiongozi wa chama cha Amani Musalia Mudavadi amemtaja Ayah kama waziri aliyejitolea kuwahudumia wananchi wakati walipofanya kazi chini katika utawala wa serikali ya rais mstaafu Daniel Moi.