Bunge la kitaifa kujadili ugavi wa bilioni 302 kwa kaunti zote

Bunge la kitaifa leo hii linatarajiwa kujadili mswada unaozitaka kaunti zote 47 nchini kugawanya bilioni 302.
Haya yanajiri baada ya bunge hilo kupendekeza kupunguzwa kwa muda wa kuchapisha mswada huo kutoka kwa siku 14 hadi 6.
Kulingana na mapendekezo ya tume ya ugavi wa raslimali za kitaifa,Shilingi Bilioni 4.1 zitaekezwa kwa hospitali kutoa huduma za bure kwa wanawake wajawazito huku shilingi milioni 900 zikitarajiwa kusaidia kununua vifaa vya hospitali.
Mswada huo pia unapendekeza shilingi bilioni nne kutengewa hospitali kuu za rufaa kisha shilingi milioni 200 zitengwe kufadhili mahitaji maalum ya matibabu.
Tayari waziri wa fedha Henry Rotich ametoa makadirio ya bajeti ya kipindi cha mwaka 2016/2017 ambayo yanatarajiwa kujadiliwa kabla ya kusomwa mwezi Juni mwaka huu.