Kongamano la mawaziri lang’oa nanga KICC

Baraza la mawaziri limeanza kongamano lake la umma rasmi asubuhi hii katika ukumbi wa mikutano wa KICC jijini Nairobi.
Kongamano hilo la siku nne litawawezesha mawaziri kuelezea hatua wizara zao zimepiga katika kutimiza ahadi ilizotoa serikali ya Jubilee wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2013.
Aidha wananchi watapata nafasi ya kuwauliza mawaziri maswali kuhusu jinsi wanavyoendesha shuguli zao katika wizara husika.