Kamati ya Elimu Kwale yatakiwa kuharakisha ufunguzi wa shule ya upili ya Mnyenzeni

 

Kamati inayoshughulikia maswala ya elimu kaunti ya Kwale imeombwa kuharakisha mikakati ya kuifungua shule ya upili ya Mnyenzeni.

Shule hiyo ilifungwa mapema wiki jana kutokana na vurugu za mara kwa mara ambazo zimekua zikishuhudiwa.

Vurugu za hivi karibuni kushuhudiwa  ni  pale kamati ya shule hiyo ilipoleta mtu anayedaiwa kuwa mganga na aliyewashurutisha wanafunzi kuaguliwa ,hatua iliiyopelekea vurugu hizo kutokana na tofauti ya dini baina ya wanafunzi.

Mjumbe wa wadi ya Kasemeni iliyoko shule hiyo Anthony  Yama anasema anaitaka kamati hiyo kufanya utatuzi wa haraka ili wanafunzi warejelee masomo yao.