Kompany nje kwa mwezi mmoja

 

Nahodha wa klabu ya Man City Vincent Kompany atakaa mkekani kuuguza jeraha kwa zaidi ya mwezi mmoja ujao.

Kocha Manuel Pellegrin amesema raia huyo wa Ubeligiji atafanyiwa uchunguzi zaidi kubaini muda halisi atakaosalia kutocheza.

Hata hivyo,Pellegrin amesema nahodha mwingine Nicholas Otamendi huenda akapatikana wikendi hii wakati vijana wake watakapochuana na Man City katika mechi ya ligi kuu EPL.

Kompany na Otamendi waliondoka uwanjani hapo jana wakati wa mechi ya kuwania taji la klabu bingwa Ulaya baina ya City na Dinamo Kiev.