FIFA yawataka maafisa wafisadi kurudisha fedha mara moja

 

 

Shirikisho la soka duniani FIFA litashurutisha maafisa walioiba fedha za shirikisho hilo kuzirudisha zote mara moja.

Rais wa FIFA Gianni Infantino amesema wameandika barua kwa idara ya Marekani inayoendesha uchunguzi dhidi ya wahusika ili kupata fedha hizo.

Infantino amesema maafisa hao zaidi ya 40 ambao tayari wamefurushwa na wanachunguzwa waliiba mamilioni ya fedha ambayo lazima watahakikisha fedha hizo zinarudi kuendeleza miradi muhimu.

Aidha Infantino ameonya kuwa katika uongozi wake hatakubali afisa yeyote kuhusishwa na ufisadi na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika.