Kaluma ataka NYS ivunjiliwe mbali

Mbunge wa Homabay,Peter Kaluma ameanzisha mchakato wa kuvunjilia mbali shirika la huduma kwa vijana yani NYS kufuatia ubadhirifu wa fedha za umma katika shirika hilo.
Kaluma ameandikia spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi barua akimwelezea nia yake ya kutunga sheria itakayofutilia mbali sheria iliyobuni NYS.
Kwenye mswada anaopendekeza Kaluma,majukumu ya NYS yatahamishwa kwa majeshi ya Kenya ili pia kupunguza gharama kwa mlipa kodi.