Rais aanzisha ziara ya siku 2 katika kaunti ya Baringo na Nakuru

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto tayari wameanza ziara ya siku mbili katika kaunti za Baringo na Nakuru asubuhi hii.
Rais atazindua mradi wa ujenzi wa bwawa la Chemususu litakaloigharimu serikali shilingi bilioni 5.5 katika eneo la Eldama Ravine kaunti ya Baringo.
Baada ya hapo rais akiandamana na viongozi kadhaa ataelelekea miji ya Molo,Njoro na Nakuru ambapo atahutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Makutano,Kamara,Total Junction miongoni mwa maeneo mengine.
Atahutubia mkutano mkuu mwendo wa 12:30 katika uwanja wa Molo kabla ya kuzindua miradi ya ukarabati wa bara bara ya Molo-Olenguruone na ile ya Nakuru-Nyahururu-Njoro-Mau Summit Junction mtawalia.
Hapo kesho,rais atakutana na viongozi kutoka kanda ya Bonde La Ufa katika ikulu ya Nakuru kisha baadaye azindue vifaa vya matibabu katika hospitali kuu ya rufaa ya Bonde La Ufa.
Rais atakamilisha ziara yake kwa kuzuru kaunti za Nyandarua na Laikipia kuzindua ukarabati wa bara bara Dundori-Oljorok na mradi wa maji jijini Nyahururu.