Erick Kiraithe ateuliwa kuwa msemaji wa serikali

 

Aliyekuwa msemaji wa polisi Erick Kiraithe ameteuliwa kama msemaji wa serikali ya kitaifa.

Naibu mkuu wa utumishi wa umma Nzioka Waita amesema uteuzi wa Kiraithe unalenga kuimarisha mawasiliano baina ya serikali na wananchi.

Katika mabadiliko hayo,sasa afisi ya msemaji wa serikali itakua chini ya wizara ya usalama wa kitaifa na masuala ya ndani.

Hata hivyo afisi ya msemaji wa Ikulu inayoshikiliwa kwa sasa na Manoha Esipisu itasalia katika afisi ya ikulu ya Rais.