Wasajili wa wapiga kura Kwale kusafiri mashinani badala ya wananchi kufika katika afisi maalum

 

Afisa mkuu wa vitambulisho katika Kaunti ya Kwale Denis Mwanza ameunga mkono kauli ya mshirikishi wa kanda ya Pwani Nelson Marwa, ya wananchi kutosafiri katika afisi za kusajili vitambulisho bali maafisa ndio wazunguke kusajili wananchi.

Akiongea na wanahabari mapema hii leo Mwanza amesema kuwa wanafuata taratibu za kuwasajili watu mashinani wala si kwa afisi,huku akitaja kuwa njia hiyo itawasaidia wananchi wenye mapato ya chini.

Kauli ya Marwa aliyoitowa wakati wa ufunguzi wa afisi ya mkuu wa wilaya huko Lunga Lunga kuwa wananchi hawapaswi kuenda Msambweni kujiandikisha kupata vitambulisho.

Aidha Mwanza ameongezea kuwa idadi ya vitambulisho walivyovitoa kwa wananchi ni kubwa na anatarajia tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuwasajili wapiga kura zaidi ya elfu 50 katika kaunti hiyo ifikapo uchaguzi mkuu wa 2017.

Mwanza ameongeza kuwa hadi kufikia sasa idadi ndogo imejitokeza kujisajili kupata vitambulisho.