Wito watolewa kwa wakaazi katika maeneo ya milima kuhamia maeneo salama Elgeiyo Marakwet

Gavana wa Kaunti ya Elgeiyo Marakwet,Alex Tolgos amewatahadharisha wakaazi wa Kaunti hiyo haswa wanaoishi katika maeneo yenye milima kuhamia maeneo salama ili kuepuka hatari ya maporomoko ya ardhi.
Tolgos amesema msimu wa mvua maporomoko hayo hushuhudiwa mara kwa mara na kupelekea hasara kubwa ya mali pamoja na kupoteza maisha ya watu.