Vijana kupata vitambulisho vya kitaifa bila vikwazo

Rais Uhuru Kenyatta amewaamrisha makamishena wa kaunti kuhakikisha vijana wanapata vitambulisho vya kitaifa mara moja bila kuwekewa vikazwo vya aina yeyote.
Rais amesema kila kijana ambaye amehitimu miaka 18 ana haki ya kupata kitambulisho cha kitaifa mahala anapoishi na sio lazima asafiri hadi pale alipozaliwa.
Akiwahutubia wananchi wa maeneo mbali mbali katika kaunti ya Isiolo baada ya kufungua kongamnao la jamii za wafugaji,Rais amewataka wananchi kujiandikisha kwa wingi kama wapiga kura ili kushiriki katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Rais amewataka viongozi wa jamii za wafugaji kushirikiana na idara za usalama kuhakikisha jamii zinaishi kwa umoja bila visa vya wizi wa mifugo ambavyo vimekua vikishuhudiwa mara kwa mara.