Mvua kali inatarajiwa katika kanda ya Pwani

Kiwango cha juu cha mvua kinatarajiwa kushuhudiwa katika kanda ya Pwani msimu huu wa masika kulingana na idara ya hewa.
Katika warsha na washikadau mbalimbali katika kaunti ya Kilifi kaimu mkurugenzi wa idara ya hali ya anga wa kaunti hiyo amesema kuwa kinyume na sehemu zingine nchini kaunti hiyo itafaidika na kiwango kikubwa cha mvua ikilinganishwa na msimu uliopita.
Aidha ameziomba idara husika kuchukua hatua mwafaka na kuona kwamba wananchi na wakulima wanafaidika na kuchukua tahadhari wakati wa msimu wa masika.
Utabiri huo umeungwa mkono na watabiri wa kitamaduni kutoka kaya za hapa Pwani hata hivyo wazee hao wamesema kuwa kutanyesha mvua kidogo mwanzo kabla ile ya masika.
Jambo lililosisitizwa zaidi na watabiri wa hali ya anga ambao wamewataka wakulima kusubiri mvua zitakazonyesha mwishoni mwa mwezi huu kwa ajili ya upanzi.