Waziri wa maji afanya ziara ya kuboresha mabwawa

Waziri wa maji Eugen Wamalwa atafanya ziara ya siku mbili katika kaunti ya Meru, ili kuboresha mabwawa ya maji pamoja na kuanzisha mikakati ya kufungua mengine.
Ziara ya Wamalwa katika kaunti hiyo inajiri siku moja tu baada ya kuzuru kaunti ya Embu na Tharaka Nithi, ambako aliboresha mradi wa unyunyizaji wa Muringa Banana ambao unatarajiwa kuongeza mazao ya wakulima.
Hatahivyo Wamalwa anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku nne katika maeneo ya Mlima Kenya hapo kesho.