Zoezi la usajili wa wapiga kura kuanza Lamu baada ya kuahirishwa

Voter-machine

Zoezi la usajili wa wapiga kura linatarajiwa kuanza hivi karibuni katika Kaunti ya Lamu na Kilifi baada ya kuahirishwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.

Katika kaunti ya Lamu zoezi hilo liliahirishwa baada ya aliyekuwa mgombea wa kiti cha ugavana Fahim Twaha kuelekea mahakamani kupinga kuchaguliwa kwa Issa Timammy kama Gavana wa kaunti hiyo.

Mshirikishi wa tume ya IEBC kanda ya kaskazini ya pwani amewataka wakaazi wa maeneo hayo kujitokeza kwa wingi ili kujisajili kuwa wapiga kura.

Haya yanajiri huku zikiwa zimesalia chini ya siku nne kwa zoezi hilo kukamilika kote nchini baada ya kung’oa nanga tarehe 15 mwezi uliopita.