Abdulswamad ashangazwa na agizo la kumtaka arudishe bastola baada ya kupokonywa mlinzi

0

Mbunge wa Mvita Abdswamad Shariff Nassir amekuwa kiongozi wa hivi punde kanda ya Pwani kupokonywa mlinzi wake wa pekee.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa Facebook Sharrif amesema kuwa ameshangazwa kuagizwa kurudisha bastola anayomiliki licha ya kuwa hana silaha hiyo.

Amesema kuwa hatatishwa na vitisho vya serikali baada ya ODM kushinda uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Malindi hivi majuzi.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya gavana wa Mombasa kupokonywa walinzi wake katika hali ya kutatanisha kufuatia kisa cha kudhalilishwa kwa mwanamke mmoja mjini Malindi.

Mshirikishi wa serikali ya kitaifa katika kanda ya Pwani alionekana kughadhabishwa na kisa hicho na kuwalaumu viongozi hao kwa kushindwa kuzuia kisa cha mama kuvuliwa nguo.