Huenda Joho na Kingi wakafikishwa mahakamani

Huenda gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho ,gavana wa Kilifi Amason Kingi na mwakilishi wa kina mama Aisha Jumwa wakafikishwa mahakamani baada walinzi wao kuhangaisha wananchi katika eneo la Malindi wakati wa uchaguzi mdogo wa eneobunge la Malindi uliokamilika hapo juzi.
Mshirikishi wa kanda za Pwani Nelson Marwa amesema kuwa walinzi wa viongozi hao waliwapiga wananchi huku wakitazama mama mmoja ambaye alivuliwa nguo na watu wasiojulikana.
Aidha Marwa amewataka maafisa wa polisi kuheshimu wananchi na kutohujuma haki zao kulingana katiba huku akimuomba inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet kuwachukulia hatua maafisa hao ambao walikiuka haki za wananchi.
Wakati huo zaidi ya watu 20 ambao ni wa kundi haramu la MRC walijitokeza na kujisalimisha huku wakiomba serikali kuwakubali waregee katika jamii.