Ripoti yaorodhesha Wabunge mabubu Bungeni

download (14)

Wabunge kutoka Pwani,Hezron Awiti wa Nyali,Gideon Mung’aro wa Kilifi Kaskazini,Masoud Mwahima wa Likoni na Gonzi Rai wa Kinango, ni miongoni mwa wabunge 27 ambao hawakuzungumza lolote bungeni mwaka jana.

Kulingana na orodha iliyotolewa na shirika huru la Mzalendo wabunge hao hawakuwasilisha mswada wa aina yeyote wala kuchangia chochote bungeni suala linaloibua maswali ni nini wanachofanya bungeni.

Orodha hiyo inaonyesha kwamba,Chiris Wamalwa wa Kiminini na Naomi Shaban wa Taveta ndio waliochangia zaidi katika bunge la kitaifa.

Mutula Kilonzo Juniour na Fatma Aden ndio maseneta waliochangia kwa asilimia kubwa katika bunge la seneti.

Hata hivyo baadhi yao wamejitokeza kukashifu ripoti hiyo wakidai hakuwashauriwa na kusema inalenga kuwadunisha mbele ya wananchi waliowachagua.