Wabunge 85 na magavana 14 kutoka jamii ya wafugaji kukutana Isiolo
Wabunge 85 na magavana 14 kutoka jamii ya wafugaji wanatarajiwa kukutana wikendi hii mjini Isiolo ili kutoa mwelekeo wa kisiasa watakaochukuwa kuanzia sasa.
Chini ya uongozi wa seneta wa Mandera Billow Kerrow na mbunge wa Samburu Kaskazini Alois Lentoimaga wamesema kwa muda maeneo ya wafugaji yanayochangia asilimia 13 ya uchumi wa Kenya yamesalia kutengwa.
Aidha mkutano huo utakaofunguliwa rasmi na rais Uhuru Kenyatta utajadili uwiano na Amani katika maeneo hayo pamoja na kuthamini utekelezaji wa ugatuzi.