Vifo vya wajawazito kupungua Lamu

Huenda visa vya kina mama wajawazito kufariki kabla na hata wakati wa kujifungua kaunti ya Lamu, vikapungua licha ya kaunti hiyo kuorodheshwa kuwa kaunti inayoongoza katika visa hivyo.

Hii ni baada ya idara ya afya na matibabu kaunti hiyo kuanzisha mradi wa ujenzi wa vituo vya kushughulikia kina mama wajawazito kabla ya kujifungua katika maeneo ambayo kina mama hao wamekuwa wakikumbwa na changamoto za usafiri.

Mkurugenzi wa huduma za afya na matibabu eneo hilo Daktari David Mulewa,amehoji kwamba, ujenzi wa vituo hivyo utasaidia pakubwa kuzuia maafa na hata kuokoa maisha ya watoto wachanga.

Mkurugenzi huyo pia amewahimiza kina mama hasa kutoka mashinani mwa Lamu kutilia maanani umuhimu wa kujifungua kwenye vituo vya afya ili kuzuia vifo na hata matitizo kutokea.