Nyumba ya gorofa 4 yaporomoka Zimmerman

Nyumba moja ya gorofa nne katika eneo la Zimmerman jijini Nairobi iliotajwa kuwa sio salama kwa wananchi kuishi imeporomoka usiku wa kuamkia leo.
Nyumba hiyo ambayo miaka 2 iliopita mamlaka ya ujenzi wa nyumba nchini NCA ilisema haifai kuwa na wapangaji imeporomoka mwendo wa saa nane asubuhi lakini hakuna yeyote alijeruhiwa.
Hata hivyo,ni bahati tukio hilo halikutokea mchana kwani lingesababisha maafa kwa wanafanyi biashara wa vyakula vya nyumbani ambao huendesha shuguli zao ndani ya jengo hilo.
NCA imeonya kwamba maelfu ya wananchi wanaendelea kuishi katika nyumba ambazo ukaguzi umeonyesha si salama kwa wapangaji japo wananchi wamesalia kimya na kudinda kuondoka.