Je,Arsenal watatamba mbele ya Barcelona bila madifenda?

arsenal-alexis-man-utd_3359505

Arsenal iko katika hatari ya kucheza mechi zake zijazo bila difenda yeyote baada ya madifenda wote kupata majeraha kufikia jana usiku.

Jana,Arsenal ikichuana na Hull City katika mechi ya kuwania taji la FA madifenda Gabriel na Per Mertesacker walijeruhiwa na sasa wanajiunga na difenda mwingine Laurent Koscienly anayeuguza jeraha.

Aidha kocha Arsen Wenger alipata pigo baada ya kiungo wa kati Aaron Ramsey pia kupata jeraha katika mechi hiyo waliopata ushindi wa mabao 4-0.

Ramsey anajiunga na viungo wengine wa kati Santi Carzola,Jack Welshere na Alex Chamberlain ambao wapo mkekani kuuguza jeraha.

Tayari kipa tegemeo Petr Cech anauguza jeraha huku kiungo mkabaji Francis Coquelin akiwa anatumikia marufuku ya kadi nyekundu.

The Gunner itachuana na Watford siku ya jumapili katika mechi ya kuwania taji la FA kisha jumatano ikabiliane na Barcelona katika mechi ya kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya.

Ukweli ni kwamba mbele ya Lionel Mess,Luis Suarez na Neymar,Nacho Monreal,Kieran Gibbs na Calum Chambers ndio watatwikwa jukumu la kuzuia safu ya difensi.

Je watafanikiwa kuwazuia MSN kupata sio zaidi ya mabao matano ugani Nou Camp?