Wanandondi 13 waondoka kuelekea Cameroon katika michuano ya kufuzu kwa Olimpiki

Wanandondi 13 wameelekea jijini Yaunde nchini Cameroon hii leo kushiriki michuano ya kufuzu katika mashindano ya Olimpiki kuanzia tarehe 9 hadi 20.
Patrick Maina na msaidizi wake David Manuhe ni wakufunzi wa timu ya wanandoni ya wanaume 10 na wanawake 3 wanao tarajiwa kufika Cameroon hii leo.
Meneja wa timu hiyo Stanley Njoroge pamoja na nahodha Nick Abaka kutoka timu ya KDF pia atashiriki mchuano huo .
Afrika wamepewa nafasi 33 za wanaume katika kila kitengo huku kina dada 3 katika uzani wa Flyweight,Lightweight na Middleweight katika michuano hiyo.