Miaka 40 gerezani kwa unyanyasaji wa kimapenzi

Mahakama moja nchini Marekani imemhukumu Mathew Durham kifungo cha miaka 40 gerezani baada ya kumpata na hatia ya kunyanyasa kimapenzi watoto katika nyumba ya watoto yatima ya Upendo kaunti ya Kiambuu.
Durhama mwenye umri wa miaka 21 ambaye ni mwanajeshi wa marekani alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa watoto saba kutoka makazi hayo ya Upendo mwaka jana bada ya kesi yake kusikizwa wilayayani Oklahama chini ya jaji Stanford Coats na baadaye kuambiwa asubiri hukumu yake amabyo imetoka leo.
Aidha wadadisi wa maswala ya kisheria awali walikuwa wamedokeza kuwa Durhama anawezapata kifungo cha miaka 30 jambo ambalo mahakama hiyo leo imeseama mshtakiwa amepewa miaka 40 ili iwe funzo kwa yeye na wengine walio na tabia kama hizo.