Mwanamume mmoja amefariki baada ya kupigwa na mwenzake kutokana na mzozo baina yao kuhusu nani mkali baina ya wachezaji Lionel Messi na Christiano Ronaldo.
Michael Chukwuma mwenye umri wa miaka 21amempiga na kumuua Obina Durumchukwu mwenye umri wa miaka 34 walipokua wakistarehe katika mkahawa mmoja jijini Mumbai nchini India usiku wa kuamkia jana.
Chukwuma ambaye ni shabiki wa Ronaldo na Durumchuku ambaye ni shabiki wa Mess walizozana hadi mmoja akamrushia mwenzake glasi iliovunjika na kumwacha na majeraha.
Kisha alichukua mabaki ya ile glasi iliovunjika alioitumia kumkata kata na kumsababishia majeraha mabaya yaliopelekea kifo chake.
Polisi wameanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji hayo ya raia wawili wa Nigeria ambayo yamewashangaza mashabiki wa soka.
Mess raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 28 anayewajibikia klabu ya Barcelona ni mshindi wa taji la Ballon d’Or mara 5.
Ronaldo raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 30 anayewajibikia klabu ya Real Madrid ni mshindi wa tuzo hiyo mara 3.