Wito watolewa kwa viongozi kuleta maendeleo badala ya kulaumiana

Viongozi mbalimbali wameombwa kujitolea ipasavyo kuleta maendeleo kwa jamii na kusahau siasa za kunyoosheana vidole vya lawama na majibizano mbele ya hadhara.
Afisa wa mipango katika shirika la Transparency International Fransis Kairu amehimiza viongozi kutekeleza majukumu kama walivyoahidi wakenya katika kampeini za uchaguzi.
Kairu ameongeza kuwa kunahaja msajili wa vyama nchini kuwachukulia hatua viongozi ambao wanatangaza kuhama vyama vyao bila ya kuzingatia sheria.