Aaron Cheruiyot wa Jubilee ndiye Seneta mpya wa Kericho

Aaron Cheruiyot amekabidhiwa rasmi cheti cha ushindi kama seneta wa kaunti ya Kericho.
Cheruiyot wa chama cha JAP ameshinda uchaguzi huo kwa kupata kura 109,358 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Paul Sang’ wa KANU aliyepata kura 56,307 pamoja na wagombea wengine watatu.
Wafuasi wa Jubilee wamesherehekea usiku kucha huku wakisubiria matokeo hayo kutoka vituo mbali mbali vya kupigia kura.
Cheruiyot amewashukura wananchi waliojitokeza kupiga kura na kuwataka aliowashinda kukubali matokeo na kufanya kazi pamoja.
Seneta wa Elgeyo Marakwet Kipchumba Murkomen,kiongozi wa wengi katika bunge la seneti Kithure Kindiki na waziri wa kawi Charlce Keter walikesha pamoja na Cheruiyot na kusherehekea pamoja wakitaja ushindi huo kuwa ishara ya umoja wa wananchi wa kanda ya Bonde la Ufa.
Hata chama cha KANU kimedinda kukubali matokeo hayo kwa madai uchaguzi haukwendeshwa kwa njia ya haki japo tume ya uchaguzi na mipaka IEBC imesisitiza kwamba uchaguzi huo uliendeshwa kisheria.