Mtengo ashinda kiti cha ubunge Malindi

William Mtengo wa chama cha ODM sasa ndiye mbunge mpya wa eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi.

Mtengo ameshinda kiti hicho katika uchaguzi mdogo kwa kupata kura 15,582 dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa chama cha JAP Philip Charo aliyepata kura 9,243.

Mgombeaji wa chama cha Labour Party Attas Ali alikua wa tatu katika uchaguzi huo akipata kura 1,547. Mutengo alikabidhiwa cheti chake cha ushindi na afisa mkuu msimamizi wa uchaguzi huo Stephene Karani.

Amewashukuru wananchi kwa kumchagua akihaidi kuwahudumia katika kipindi cha uongozi kilichosalia.

Tume ya IEBC imesema licha ya uchaguzi huo kukumbwa na changamoto mbali mbali,uliendeshwa kwa njia iliyostahili.