Washukiwa 4 wa ugaidi waliokamatwa wakielekea Libya wafikishwa mahakamani

 

images (9)

Washukiwa wanne wa ugaidi wametupwa korokoroni kwa siku 30 baada ya kufikishwa mahakamani mjini Mombasa mapema leo, baada ya kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi katika boda ya Busia hapo jana.

Wanne hao wanasemekana walikuwa wanapania kusafiri hadi nchini Libya kwenda kujiunga na kundi la ISIS kupitia kaunti hiyo ya Busia kabla ya njama yao kutibuka.

Haya yanajiri wakati ambapo maafisa wa usalama wanazidi kukaza kamba dhidi ya visa vyovyote vya utovu wa usalama hususan baada ya vitisho vipya kutoka kwa wanamgambo wa Alshabab.