Wenger atoa onyo kwa mashabiki wanaowakejeli wachezaji wanapolemewa

Kocha Arsen Wenger amewaonya mashabiki wa klabu ya Arsenal dhidi ya tabia yao kupiga kelele za kuwakejeli wachezaji wanapolemewa uwanjani.
Mfaransa huyo amesema iwapo tabia hiyo itaendelea,huenda ikaathiri matokeo ya Arsenal na sasa anawataka kukoma mara moja.
Wenger amekashifu hatua ya mashabiki wa Arsenal kusherehekea wanapopata ushindi lakini kuwatukana wachezaji wanapokosa ushindi akisema suala hilo halifai kamwe mchezoni.
Mashabiki wa Arsenal walijipata pabaya jumamosi baada ya kelele zao kuzimwa na Alexis Sanchez aliefunga bao kulazimisha sare ya mabao 2-2 na Tottenham Hotspurs katika mechi walionekana kupoteza.