Shujaa yaandikisha matokeo mchanganyiko Las Vegas

 

download (7)

Timu ya taifa ya raga wachezaji saba upande imezoa alama 10 katika makala ya 5 kuwania taji la dunia la HSBC World Series yaliokamilika hapo jana jijini Las Vegas nchini Marekani.

Shujaa ilibanduliwa katika hatua ya nusu fainali kuwania taji la Plate baada ya kutandikwa alama 19-14 na Japan.

Hii ni baada yao kubanduliwa nje ya taji kuu katika hatua ya robo fainali kwa kutandikwa alama 26-14 na Marekani inayoongozwa na kocha Mike Friday.

Shujaa Vijana walivuna ushindi katika mechi za awamu ya makundi wakimpiga Urusi alama 24-21,Ureno 38-0 na New Zealand alama 22-0 mtawalia.

Fiji waliibuka washindi wa taji kuu baada ya kuigaragaza Ausralia alama 21-15 katika fainali.

Sasa Kenya inashikilia nafasi ya 8 katika jedwali la dunia kwa alama 52 ambapo inajiandaa kwa makala ya 6 nchini Canada.