Polisi wachunguza madai ya hongo kwa wapiga kura Malindi

Maafisa wa polisi wanachunguza madai ya hongo kwa wapiga kura yanayohusishwa na baadhi ya wabunge wakati wa zoezi la uchaguzi mdogo wa Malindi unaoendelea.
Katika moja ya matukio hayo maafisa hao walilazimika kupiga risasi hewani ili kutawanya kundi la vijana waliokuwa wanamvamia mbunge wa Lamu Mashariki Sharif Athman kwa madai ya kununua wapiga kura.
Mbunge wa Kabete Ferdnand Waititu pia alijipata matatani kufuatia shutma hizo pamoja na mbunge wa Mwea Peter Gitau miongoni mwa wengine.