Uchaguzi Malindi na Kericho waendelea

Wagombea 6 wanawania kiti cha useneta katika kaunti ya Kericho.
Japo siasa zilisheheni wagombea wawili wakuu,wapo wengine wanne ambao wanashiriki uchagzui huo.
Aaron Cheruiyot wa chama cha Jubilee na Paul Sang’ wa KANU ndio wanapigiwa upato kunyakua kiti hicho kutokana na kampeni kali zilizoendeshwa baina ya viongozi wa vyama hivyo.
Naibu rais William Ruto ambaye kwa muda amekua kigogo cha kanda ya Rift Valley anakabiliwa na upinzani wa kudhibitisha iwapo bado yeye ni kigogo atakapokumbana na wimbi kali la viongozi wasai wa Jubilee walioungana na viongozi wa KANU katika eneo hilo.
Wycliffe Kipkemoi,Paul Sigei,Daniel Tunoi,David Mutahi miongoni mwa wengine.
Gavana wa Bomet Isaac Ruto na mwenyekiti wa chama cha KANU Gideon Moi wameendesha kampeini dhidi ya Jubilee wakiwataka wananchi kumchagua Paul Sang’ wakidai serikali haijatimiza ahadi kwa wananchi.
Huko Malindi wagombea 5 wameidhinishwa kushiriki uchaguzi huo japo kivumbi ni baina ya Philip Charo wa Jubilee na Williy Mutengo wa ODM.
Jubilee imewategemea wabunge waasi wa ODM Gideon Mung’aro,Khatibu Mwashetani,Mustapha Idd na Zeinab Chidzuga kuhakikisha Charo anaibuka mshindi na kutwaa kiti hicho kilichoshikiliwa na ODM hapo awali.