SRC yaanza rasmi zoezi la kutathmini kazi za walimu

srcchair

Tume ya kudhibiti mishahara nchini inatarajiwa kuanza rasmi zoezi lake la kutathmini kazi za walimu katika kaunti zote 47 nchini.

Mwenyekiti wa tume hiyo Sara Serem anatarajiwa kuongoza zoezi hilo katika kaunti ya Kwale mapema leo kabla kuelekea katika shule ya Star Of The Sea mjini Mombasa hapo kesho kwa ushirikiano na tume wa kuwaajiri walimu TSC.

Haya yanajiri huku walimu hao wakiapa kutoshiriki zoezi hilo kwa madai kwamba linapania kutatiza na kuchelewesha mazungumzo kuhusu nyongeza ya mishahara kati yao na waajiri wao.

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion amesema kuwa watakabiliana vilivyo na yeyote atakayewashurutisha kushiriki zoezi hilo kwa kuwa hawalitambui.