Moto mkali wazuka katika bunge la Makueni

Majengo ya bunge katika kaunti ya Makueni yameteketea moto baada ya moto kuzuka katika majengo hayo mapema hii leo.
Kiongozi wa waliowengi katika bunge hilo Francis Mutuka amesema kuwa maliĀ ya mamilioni ya pesa yameharibiwa na moto huo ambao chanzo chake hakijajulikana.
Aidha Mutuka amesema kuwa moto huo haujakabiliwa kufikia sasa kwasababu kaunti hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa gari za kuzima moto.