Idadi chache yajitokeza kupiga kura Malindi

Mgombea kiti cha eneo bunge la Malindi kwa tiketi ya Jubilee Phillip Charo tayari amepiga kura yake katika shule ya msingi ya Maziwani.
Haya yanajiri huku idadi ndogo ya wapiga kura ikisemekana kujitokeza hadi sasa katika zoezi hilo lililong’oa nanga muda mfupi baada ya mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi.
Hakuna visa vyovyote vya utovu wa usalama vilivyoripotiwa hadi sasa huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika mwendo wa saa kumi na mbili jioni.