Shujaa yafuzu robo fainali Las Vegas

Timu ya taifa ya raga wachezaji saba upande imefuzu robo fainali kuwania taji la dunia la IRB Sevens katika makala ya 5 yanayoendelea jijini Las Vegas kwa sasa.
Kenya imeitandika Urusi alama 24-21 katika mechi ya ufunguzi kasha ikailemaza Ureno alama 38-0 katika mechi ya pili. Sasa Shujaa watachuana na New Zealand katika mechi ya tatu kabla ya droo ya robo fainali kufanyika.
MATOKEO
New Zealand 42-07 Ureno,Afrika Kusini 33-07 Canada,Marekani 19-12 Wales,Fiji 24-28 Samoa, Argentina 26-07 Ufaransa, Australia 26-07 Scotland,Uingereza 19-19 Japan,New Zealand 38-0 Urusi ,Marekani 26- 26 Canada