Sossion na Mudzo wahifadhi wadhifa wao

download (16)

Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini KNUT Wilson Sossion pamoja na mwenyekiti wake Mudzo Nzili wameteuliwa bila kupingwa katika uchaguzi wa kamati simamizi wa chama hicho uliofanyika leo jijini Nairobi.

Zoezi hilo limefanyika katika uwanja wa Kasarani gymnasium huku walimu hao wakipata nafasi ya kuwachagua maafisa katika nafasi za katibu mkuu na mwenyekiti wao ambapo wawili hao wamehifadhi viti vyao kwa mara nyengine bila kupingwa.

Uchaguzi huu unafuatia chaguzi mbalimbali zilizoandaliwa kwenye kaunti zote 47 ambako wanachama walikuwa wakiwachagua viongozi wao mashinani.